The Dady D Blog:

Filamu ya Hollywood iliyochukua bajeti kubwa sana ikiwa na
jina la ‘Noah’ ambayo imeigizwa na Russell Crowe kama Nuhu imepigwa
marufuku kuoneshwa katika nchi wanachama wa Umoja wa nchi/Falme za
Kiarabu (United Arab Emirates).
Filamu hiyo imepigwa marufuku kwa madai kuwa kwanza inazua mtazamo
tofauti kutokana na utofauti uliopo kati ya Biblia na Quran kuhusu
simulizi la Nuhu na gharika ingawa kuna mfanano katika vitabu hivyo
vitakatifu kuwa kulitokea mafuriko na Mungu akamwambia Nuhu ajenge
safina.
Sababu ya pili ni kuonesha mfanano wa nabii na muigizaji wa kawaida
hali inayoweza kuzua hisia tofauti kwa baadhi ya waumini wa dini ya
kiislamu.
Mkurugenzi wa maudhui ya vyombo vya habari wa umoja wa nchi/falme za
Kiarabu (National Media Centre-United Arab Emirates), Juma Al-Leem,
ameiambia Associated Press kuwa filamu hiyo haitaruhusiwa kwenye nchi
hizo kwa kuwa inakinzana na miiko katika dini ya kiislam hasa katika
kumfananisha nabii na mtu wa kawaida.
“Kuna vipande vya filamu hiyo ambavyo vinakanganya (simulizi) kati ya
Biblia na Uislam, kwa hiyo tumeamua kuacha kuionesha.” Alisema Juma
Al-Leem. “Ni muhimu kuheshimu dini hizi mbili na kuacha kuonesha filamu
hiyo.
Taasisi ya kiislamu ya Al-Azhar ya Misri, imeeleza kuwa imeikataa
filamu hiyo kwa kuwa iko kinyume na mafundisho ya dini hiyo na kwamba
kuonekana kwa kukataa kuonesha taswira ya mtu ikifananishwa na ile ya
nabii kutasaidia kuepuka watu kuanza kumuabudu mtu badala ya Mungu.
No comments:
Post a Comment