The Dady D Blog
Chriss brown ametupwa jela baada ya kukiuka agizo ya jaji la kuendelea kukaa Rehab. Ijumaa asubuhi, muimbaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alifukuzwa kwenye Rehabu hiyo iliyopo Malibu nchini marekani ambako amekaa kwa karibu miezi minne
Jaji anayesimamia Kesi yake ya kumpiga Rihanna, alimuagiza Brown kuendelea kukaa Rehab kwa siku 90 ili kusaidiwa kupunguza hasira ambako alimaliza mapema mwezi huu. Hata hivyo mwishoni mwa mwezi uliopita jaji huyo aliamuru msanii huyo aendelee kukaa Rehab kwa miezi mingine miwili.
Haijulikani kwanini amefukuzwa rehab lakini mtandao wa TMZ umedai kuwa amekiuka baadhi ya sheria za ndani japokuwa hazihusiani na madawa ya kulevya au fujo
No comments:
Post a Comment